Breaking News

header ads

MWILI WA MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI WAOKOTWA MTONI

Mwili wa marehemu ukielea mtoni huku ukiwa kwenye viroba.

MWILI wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah,  unadaiwa umekutwa na wavuvi mto Ndabaka eneo la Bunda – Lamadi akiwa amefariki dunia jana Jumatano, Machi 14,2018 jioni huku watu wa karibu na marehemu wakithibitisha kuwa mwili huo ni wake.
Samson Josiah anayedaiwa kuuawa.
Machi 9, 2018 taarifa za kupotea kwa Josiah kwa zaidi ya wiki mbili zilianza kusambaa baada ya gari lake alilokuwa akitumia aina ya Toyota Land Cruiser kukutwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara huku  akiwa hajulikani alipo.
Gari lake lilivyokutwa limechomwa moto.


Post a Comment

0 Comments