Breaking News

header ads

Ajali mbaya ya Helikopta iliyotokea jijini New York jana tarehe 12 march 2018

"Ajali mbaya ya Helikopta iliyotokea jijini New York nchini Marekani inaweza kuwa imesababishwa na mzigo wa abiria." alieleza Rubani alipohojiwa na wapelelezi.
Rubani huyo alisema kuwa huenda moja ya mizigo ya abiria iliponyeza kitufe(button) cha dharura ya mafuta, na kusababisha ajali hiyo iliyoua abiria wote watano isipokuwa rubani, kwa mujibu wa maelezo ya Afisa mkuu wa utekelezaji wa sheria.
Abiria walikua katika shughuli binafsi ya kufanya Photoshoot katika helikopta hiyo ya Liberty(kampuni) na chanzo cha polisi kilibainisha kuwa rubani Richard Vance ni mwenye umri wa miaka 33.
Waathirika wote walikuwa kati ya umri wa miaka 26 na 34, kulingana na Idara ya Polisi ya New York.
Helikopta iliondolewa majini siku ya Jumatatu mchana na inachunguzwa na wataalam kutoka Bodi ya Usalama wa Taifa ya Usafiri, mwanachama wa NTSB Bella Dinh-Zarr alisema.
Wachunguzi watakagua helikopta, vifaa vyake vya kuelea, hali ya hewa na mambo mengine katika shughuli ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Msemaji wa Marekani Chuck Schumer wa New York aliwaita FAA kusimamisha cheti cha uendeshaji wa FAA ya Helikopta za Liberty mpaka rekodi ya usalama wa kampuni na ajali hii itakapodhibitishwa kikamilifu.

VIDEO FUPI YA TUKIO HII HAPA CHINI


Post a Comment

0 Comments